MATAJIRI wa Dar, Azam FC hesabu kubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wao wa mwisho msimu wa 2024/25 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Azam FC uwanja wao wa nyumbani ni Azam Complex wanafunga ukurasa wa mwisho kwa mchezo dhidi ya TaboraUnited katika msako wa pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.
Kwenye msimamo Tabora United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 37 baada yakucheza mechi 28 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo.
Azam FC ina pointi 57 baada yakucheza jumla ya mechi 28. Timu zote mbili zipo ndani ya tano bora ndani ya msimu wa 2024/25.
Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo wa funga kazi wakiwa nyumbani hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi Juni 18 2025 saa 10:00 jioni.
Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Azam FC kucheza saa 10:00 jioni wakiwa Uwanja wa Azam Cmplex kwa kuwa mara nyingi ratiba yao ilikuwa ni saa 1:00 usiku kutokana na uwepo wa taa bora katia uwanja huo ambao ni bora Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.