KIUNGO wa mpira ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi amerejea kazini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kukamilisha mzunguko wa pili 2024/25.
Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 73 baada ya mechi 27 ni mechi tatu zimebaki kwa mujibu wa ratiba huku wao wakibainisha kuwa wamebakiwa na mechi mbili.
Mechi ambazo Yanga SC imebainisha kuwa zimebaki kwa mujibu wa ratiba yao ni dhidi ya Tanzania Prisons, Dodoma Jiji huku mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC ambao umepangwa kuchezwa Juni 15 wakiwa hawajaubainisha kwenye ratiba zao.
Kiungo ambaye amerejea kwenye eneo la uwanja wa mazoezi ni Khalid Aucho huyu ni kiungo mkabaji ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union dakika ya 44 nafasi yake ilichukuliwa na Mudathir Yahya.
Kwa mujibu wa Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa wachezaji ambao wapo kambini wote wapo fiti kwa maandalizi ya mechi zilizobaki.
“Wachezaji ambao wapo kambini ikiwa ni pamoja na Khalid Aucho wapo tayari kwa ajili ya mechi zetu zilizobaki kukamilisha msimu wa 2024/25.”
Mchezo wa Yanga SC dhidi ya Tanzania Prisons unatarajiwa kuchezwa Juni 18 2025 itakuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.