YANGA YAFUNGA MJADALA KARIAKOO DABI

RASMI Uongozi wa Yanga umetangaza kufunga mjadala wa kuzungumzia kucheza mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba ambao ulihairishwa na Bodi ya Ligi Kuu Bara ambao umepangwa kupigwa Juni 15, mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar.

“Sisi tuna mawasiliano na bodi ya ligi, kuelekea dabi sisi tumeshatoa msimamo wetu na tumeshaweka ‘fixtures’ zetu za kumaliza msimu huu. Huu mjadala umeshafungwa na itakuwa vibaya sisi kurudiarudia kitu kilekile.

“Sisi hatuihofii Simba, wala timu yoyote ile kwa sababu sisi ndiyo tunaongoza ligi na tunaweza kufunga timu yoyote. Tuendelee kula mtori na uzuri kwa sasa tunadili na watu wengi,” alisema Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ali Kamwe.