UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kuwa mpango mkubwa kuelekea kwenye mchezo wa fainali wa CRDB Federation Cup jambo kubwa ambalo wanahitaji ni ubingwa.
Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi itamenyana na Singida Black Stars kwenye fainali inayotarajiwa kuchezwa Zanzibar.
Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi walitwaa taji hilo kwa ushindi mbele ya Azam FC ambayo msimu huu haijafika hatua ya nusu fainali.
Singida Black Stars iliwaondoa Simba SC hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa malengo makubwa ni kupata ushindi kwenye kila fainali ambayo wanacheza.
“Ikiwa kuna fainali halafu kuna kombe basi hakuna namna Yanga SC tunaiweza kazi hiyo na malengo ni kuona tunatetea taji letu, tupo tayari na mashabiki wawe pamoja nasi.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.