JEAN AHOUA ANAWINDWA KIMATAIFA

KIUNGO mshambuliaji namba moja wa Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Jean Ahoua anatajwa kuwindwa na timu kubwa Afrika.

Ahoua ni chaguo la kwanza la Fadlu kutokana na uwezo alionao huku mguu wake wenye nguvu ukiwa ni ule wa kulia.

Nyota huyo ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika amefunga jumla ya mabao 15 na pasi 8 za mabao akiwa ni kinara kwenye chati ya ufungaji.

Mabao yote ambayo amefunga asilimia 99 ni mguu wa kulia ambapo kafunga kwa mguu wa kulia jumla ya mabao 14 na kafunga bao moja kwa pigo la kichwa.

Inatajwa kuwa Ahoua yupo kwenye rada za mabosi wa Kaizer Chiefs ambao wanahitaji huduma ya kiungo huyo aliyefunga bao pekee kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Uwanja wa New Amaan Complex.

Simba SC kutoka Tanzania wamegotea kuwa washindi wa pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na mabingwa ni RS Berkane.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.