KOCHA Mkuu wa Simba raia wa Afrika Kusini, Fadlu Davis amesema kamwe hawatakubali kufungwa mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga utakaopigwa Juni 15, mwaka huu.
Fadlu alisema kuwa mchezo huo ndiyo utahamua hatima ya wao kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo hawatakubali kufanywa daraja la ubingwa katika msimu huu.
“Tunakwenda mapumziko tukipisha kalenda ya Fifa ya timu za taifa kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa, lakini tutarejea haraka kuanza maandalizi ya dabi ambayo lazima tuwafunge Yanga,” alisema Fadlu.