DICKSON JOB KIMEELEWEKA YANGA, APEWA MIAKA MIWILI

KLABU ya Yanga imefikia makubaliano mazuri ya kumuongezea mkataba mwingine beki na nahodha wake msaidizi, Dickson ‘Dick’ Job.

Inealezwa makubaliano hayo yaliyofikiwa ya miaka miwili kwa dau na mshahara mnono aliouongezewa katika mkataba huo mpya.

Beki huyo muda wowote anatarajiwa kusaini mkataba huo mpya huku akiandaliwa utambulisho mkubwa wa kumbakisha beki huyo aliyekuwa anatajwa kwenda Simba msimu ujao.