UONGOZI wa Yanga umeibuka na kusisitiza kuwa hawatacheza mchezo wa Kariakoo Dabi uliopangwa kuchezwa Juni 15, mwaka huu dhidi ya Simba .
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa wao wanachojua wamebakisha michezo miwili ya Ligi Kuu Bara na siyo mitatu .
“Akili yetu imejikita kwenye kuzimaliza kwa kishindo mechi zetu mbili za Ligi Kuu Bara zilizobaki dhidi ya Tanzania Prisons na Fountain Gate pekee,” alisema Kamwe.
BOSI YANGA ASISITIZA KUTOCHEZA KARIAKOO DABI
