BEKI wa Simba SC, Che Malone anatajwa kuwa kwenye hesabu za kukutana na mkono wa Thank You kutokana na kiwango chake kuporomoka kwa mara nyingine tena.
Beki huyo ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids mara baada ya kurejea kutoka kutokuwa fiti baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Azam FC, mwendo wake haujawa bora kwenye mechi za ushindani.
Katika mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane aliingia baada ya beki Hamza Jr kupata maumivu kipindi cha kwanza na alikamilisha dakika ambazo zilibaki bila timu hiyo kufungwa bao jingine kwa kuwa wakati anaingia ubao ulikuwa unasoma RS Berkane 2-0 Simba SC.
Fainali ya pili Tanzania baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-1 RS Berkane na ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika ukawa mali ya RS Berkane.
Kazi ilikuwa nzito kwenye nusu fainali ya CRDB Federation Cup, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-3 Singida Black Stars.
Simba SC ilifungashiwa virago mbele ya Singida Black Stars huku safu ya ulinzi ikifanya makosa kwenye kuokoa hatari ndani ya 18 jambo lililofanya timu hiyo ikafungwa.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Simba SC wanaangalia namna bora yakuboresha eneo la ulinzi huku beki Che Malone akiwa ni miongoni mwa mabeki wanaotazamwa kwa ukaribu ikiwa watapata mbadala wake huenda akapewa Thank You ama akaongezewa muda kwa makubaliano maalamu hasa kuboresha kiwango chake.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.