Ally Salim kipa namba mbili wa Simba SC yupo kwenye mtego ndani ya kikosi hicho kutokana na mwendo wake kutokuwa imara.
Kwenye msimu wa 2024/25 ndani ya Ligi Kuu Bara, Ally amekaa langoni kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 alifanikiwa kukamilisha dakika hizo na hati safi.
Kwenye mchezo mmoja wa CRDB Federation Cup ilikuwa ngumu kwake kutoka na hati safi alipotunguliwa mabao mawili na Emannuel Kwame wa Singida Black Stars.
Alipachika bao moja kwa pigo huru akiwa nje kidogo ya 18 na alipachika bao moja kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 baada ya Ally kutoa pasi ambayo haikufika kwa mchezaji wa Simba SC.
Kipa huyo alifunga Mei 2025 kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ukisoma Simba SC 1-3 Singida Black Stars.
Bao moja lilifungwa na Jonathan Sowah ambaye alimtungua kipa namba moja wa Simba SC, Moussa Camara ambaye alikwama kukamilisha dakika 90 baada yakupata maumivu kwenye mchezo huo.
Simba SC imefungashiwa virago kwenye CRDB Federation Cup ni Yanga SC vs Singida Black Stars hawa watacheza fainali.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.