SIMBA SC 1-3 SINGIDA BLACK STARS CRDB FEDERATION CUP, MEI 31 2025

SINGIDA Black Stars imekata tiketi ya kucheza fainali kwa CRDB Federation Cup kwa ushindi wa mabao 3-1 mbele ya wenyeji wao Simba SC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Mei 31 2025.

Singida Black Stars walianza kwa hesabu ndani ya dakika 20 walipopata bao la kuongoza kupitia kwa Jonathan Sowah dakika ya 17.

Dakika ya 35 Emmanuel Kwame ambaye amechaguliwa kuwa mchezaji bora hatua ya nusu fainali alipachika bao la pili na akapachika bao la tatu kwa pigo la faulo dakika ya 49.

Bao pekee la Simba SC limefungwa na Jean Ahoua dakika ya 68. Huu ni mchezo wa funga Mei 2025 kwa timu zote mbili ambapo Simba SC imeonja joto ya jiwe.

Licha ya wachezaji chaguo la kwanza ikiwa ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr na Ellie Mpanzu kuingia kipindi cha pili bado ukuta wa Singida Black Stars chini ya Kennedy Juma ulikuwa imara haukuruhusu kufungwa mabao zaidi ya mawili.

Mpanzu kwenye mchezo wa leo alimchezea faulo Kennedy Juma na alionyeshwa kadi ya njano na Ahmed Arajiga dakika ya 50. Makipa wote wa Simba SC wamefungwa alianza Moussa Camara ambaye alifungwa bao moja na Ally Salim akafungwa mabao mawili.

Fainali ni Yanga SC vs Singida Black Stars itakayoamua bingwa wa CRDB Federation Cup. Ikumbukwe kwamba bingwa mtetezi ni Yanga SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.