KIUNGO mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Wydad Casablanca, Aziz Ki tayari ameanza mazoezi na timu hiyo mara baada ya kumtambulisha.
Ikumbukwe kwamba Ki aliibuka ndani ya timu hiyo akitokea kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Mchezo wa mwisho akiwa na uzi wa Yanga SC ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania ambao ulikuwa ni CRDB Federation Cup hatua ya nusu fainali.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya dakika 90 ubao ukasoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.
Mei 25 alitambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Wydad Casablanca kiungo huyo mshambuliaji ambaye alikuwa anavaa jezi namba 10 ndani ya kikosi cha Yanga SC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.