MTENDAJI Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, maarufu kwa jina la Popat baba yake mzazi ametangulia mbele za haki Mei 23 2025.
Taarifa iliyotolewa na Azam FC imeeleza namna hii: Asalaam Aleykum wa Rahmatullahi wa Barakatuhu!
“Kwa masikitiko makubwa, Azam FC inatangaza kifo baba mzazi wa Mtendaji wetu Mkuu (CEO), Abdulkarim Amin ‘Popat’, Mzee MohamedAmin Nurdin Haldey, kilichotokea alfajiri ya leo Ijumaa, Hospitali ya Aga Khan.
“Mwili wa marehemu utaswaliwa msikiti wa Maaamur, Upanga – Dar es Salaam, baada ya swala ya Ijumaa, na mazishi yatafanyika kwenye makaburi ya Kijitonyama barabara ya Rose Garden.