TOTTENHAM WATWAA TAJI LA EUROPA LEAGUE MBELE YA MANCHESTER UNITED

TOTTENHAM chini ya Kocha Mkuu,Gregg Popovich wametwaa taji la Europa League kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United kwa bao pekee la Brennan Johnson dakika ya 42 ndani ya Uwanja wa San Mames na timu hiyo itacheza Champions League.

Katika mchezo huo wa fainali, rekodi zinaonyesha kuwa shuti ambalo walipiga Spurs lango la Manchester United likalenga lango ni moja ambalo lilikuwa bao la ushindi katika mchezo huo.

Manchester United ni mashuti matatu walipiga langoni hayo yote yaliokolewa na kipa wa Tottenham kwenye fainali hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Umililiki wa wa mpira ilikuwa ni asilimia 35 kwa Tottenham na Manchester United walikuwa na asilimia 65 za umiliki.

Faulo ilikuwa 20 kwa Tottenham na 9 ilikuwa ni kwa Manchester United. Kadi za njano mastaa wa Tottenham watatu walionyeshwa na wanne kwa upande wa Man United.

Hakukuwa na kadi nyekundu kwenye fainali na kuotea ni mara moja kwa Tottenham huku Man United wakikutwa katika mtego mara mbili.

Mapigo ya kona ni nne kwa Tottenham na 5 kwa Manchester United. Shukrani kwa mlinda mlango Guglielmo Vicario ambaye aliokoa hatari nne kwa Tottenham na Andre Onana wa Manchester United akitunguliwa bao moja.

Walioonyeshwa kadi za njano kwa upande wa Tottenham ni:-Yves Bissouma dakika ya 68, Richarlison dakika ya 58 na Micky Van de Ven dakika ya 49.

Manchester United ni Amad Diallo ilikuwa mapema kipindi cha kwanza dakika ya 35, Joshua Zirkzee dakika ya 84, Harry Maguire dakika ya 88 na Johnny Evans dakika ya 90.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka na mtandao, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.