ISHU YA KIPA BORA YANGA SC YAMALIZA UTATA

UONGOZI wa Yanga SC umebainisha kuwa uwepo wa Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja kwenye timu hiyo kunaongeza somo kwa timu nyingine kutambua namna gani mlinda mlango bora anakuwa.

Diarra msimu wa 2024/25 ni namba mbili kwa makipa ambao wamekusanya hati nyingi safi, (clean sheet) akiwa nazo 15 kinara ni kipa wa Simba SC, Moussa Camara ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Kipa huyo amekaa langoni kwenye jumla ya mechi 21 akikomba dakika 1,890 katunguliwa mabao 8 akiwa na wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 236.

Camara wa Simba SC amekaa langoni kwenye 24 akikomba dakika 2,160 akiwa katunguliwa mabao 11 wastani wakutunguliwa bao moja kila baada ya dakika 196 hajafungwa kwenye mechi 16.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua kuna suala ambalo lipo kwenye eneo la walinda mlango kufanya kazi zao huku Diarra akitoa somo kwa makipa wengine.

“Unajua ukimuangalia Diarra yeye anatoa somo kwa timu nyingine kuona namna gani anakuwa na kipa bora, sio kila kipa anastahili kuwa kipa bora ila Diarra yeye anaonyesha ubora zaidi ulivyo kwa kutimiza majukumu yake uwanjani.

“Unaona kwa sasa amefikisha jumla ya hati safi 15 hii inaonyesha anaendeleza ubora wake akiwa kwenye majukumu yake bado kuna somo ambalo linatolewa kwa timu nyingine kujua namna gani zitapata mlinda mlango.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.