SIMBA YATANGAZA VIINGILIO VYA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA NA KUZINDUA HAMASA KWA MASHABIKI

“Tunataka kufanya fainali yenye hadhi ya juu mno, na hayo ni mambo ambayo sisi tunayamudu. Ndugu zangu fainali ndio hatua ya juu kabisa ya mashindano. Kuelekea katika mchezo huu tunatangaza viingilio na tutakaporudi kutoka Morocco tutazindua hamasa. Napenda kuwasihi Wanasimba kununua tiketi mapema. Mwakani tutacheza tena fainali lakini haitakuwa kama hii ambayo tumeisubiri kwa miaka 30.”

“Viingilio ni;
Mzunguko – Tsh. 7,000.
VIP C – Tsh. 20,000.
VIP B – Tsh. 30,000.
Platinum – Tsh. 250,000.

Anayetaka Platinum ana dakika zisizozidi 60 kuwahi. Hakutakuwa na daraja VIP A sababu baadhi ya wageni wa CAF watakaa eneo hilo. Wale wanangu wa VIP A wahamie eneo la VIP B au VIP B.”

“Tunazungumza na wenzetu wa N-Card kuweka wauza tiketi katika maeneo ambayo yanaonekana hayana wauzaji wengi wa tiketi. Mfano ukanda wa Tabata kuweka mtu wa tiketi. Tutasambaza mawakala wa tiketi katika kona mbalimbali za Dar es Salaam ili Wanasimba wanunue tiketi kwa urahisi.”

“Kuna watu wanatoka nje ya Tanzania kuja kuangalia fainali hii sasa Wanasimba mliopo hapa changamkieni nafasi hii. Kuepuka usumbufu Mwanasimba nunua tiketi yako mapema.”- Semaji Ahmed Ally.