KMC: TUMEHARIBU HATI SAFI YA CAMARA, BAHATI YAO

UONGOZI wa KMC FC umebainisha kuwa bahati ilikuwa upande wao Simba SC kupata matokeo kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Mei 8 2025 wakipoteza pointi tatu.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma KMC FC 1-2 Simba SC, mabao yalifungwa na Rashid Chambo dakika ya 8 kwa upande wa KMC huku yale ya Simba SC yakifungwa na Steven Mukwala dakika ya 15 na 47 akifikisha mabao 11 kwenye ligi.

Mukwala alifunga mabao hayo akitumia pasi kutoka kwenye miguu ya Joshua Mutale ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

Khalid Chukuchuku, Ofisa Habari wa KMC amebainisha kuwa walicheza kwa umakini mkubwa walikosa nafasi kuzitumia jambo ambalo limewapa matokeo mabaya.

“Ilikuwa ni bahati kwa upande wa Simba SC kwa kuwa tulikuwa na uwezo wakushinda mchezo hasa kipindi cha kwanza na kipindi cha pili kuna nafasi ambazo tulikosa kufunga jambo ambalo wapinzani wetu walizitumia.

“Tunawapongeza wachezaji kwa namna walivyopambana kusaka pointi tatu na kukwama ila tumetibua rekodi ya kipa Moussa Camara kuondoka na hati safi kwenye mchezo wetu ambao tulikuwa tumeukamata kwa asilimia kubwa.”

KMC kwenye msimamo ipo nafasi ya 11 ikiwa na ponti 30 baada ya mechi 27, vinara ni Yanga SC wenye pointi 70 baada ya mechi 26 wanafuatiwa na Simba SC nafasi ya pili wakiwa na pointi 69.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.