BAADA ya Kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo kupokelewa sokoni kwa mikono miwili kikiingia kwenye orodha ya vitabu vilivyokubalika ndani ya Septemba kuna kazi mpya nyingine inakuja kutoka kwa mtunzi chipukizi ambaye yupo kwenye mikono ya Mtunzi bora wa muda wote Eric Shigongo.
Ikumbukwe kwamba Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ilizinduliwa Septemba 24 2024 makao makuu ya Global Group sasa ni kazi mpya inayokwenda kwa jina la Moyo Wangu Unavuja Damu, hivi vyote vimeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka.
Kitabu cha Moyo Wangu Unavuja Damu rasmi kitazinduliwa Julai 24, 2025, Sinza Mori, Dar es Salaam. Ni wakati mwingine kwa wasomaji na Watanzania kupata mwendelezo wa kazi nzuri kutoka kwa mtunzi Lunyamadzo Mlyuka.
Hii ni aina ya simulizi ambayo inakwenda kuzungumzia maisha ya Mtanzania ambaye anapambania malengo yake kwa udi na uvumba huku akipambana na vikwazo vilivyokuwa njiani mwake mwisho vizingizti hivyo vilimpa kesi nzito ambayo yeye mwenyewe aliona inamshinda.
Usikubali kuikosa kwani kuna masuala ya usaliti, furaha, familia huku ikiwa imebeba madhari halisi ya Afrika.
Ninaomba oda yako kwa Soft Copy na Hard Copy kupitia namba hii +255 756 028 371, email 📧thisisdizo444@gmail.com.