ORODHA YA VINARA KWENYE UTUPIAJI LIGI KUU BARA

KAZI bado inaendelea ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora kwa kila timu kupambania kufikia malengo kukamilisha mzunguko wa pili 2024/25.

Katika eneo la ushambuliaji kuna orodha ya mastaa ambao ni wakali kwenye eneo la kucheka na nyavu waliopo kwenye vita ya kuwania tuzo ya kiatu cha ufungaji bora.

Hapa tunakuletea wakali kwenye kucheka na nyavu namna hii:-

Jean Ahoua- 15

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids rekodi zinaonyesha kuwa amecheza mechi 23 akikomba dakika 1,689. Ahoua Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mabao 15 ambayo kafunga, mabao 14 katupia kwa mguu wa kulia huku bao moja akifunga kwa pigo la kichwa ilikuwa mchezo dhidi ya Pamba Jiji alipotumia pasi ya Ellie Mpanzu Uwanja wa KMC Complex.

Clement Mzize-13

 Clement Mzize mali ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Mzize katupia jumla ya mabao 13 katika mchezo dhidi ya Fountain Gate alipachika mabao mawili nakufikisha mabao 13. Yanga SC imetupia jumla ya mabao 68 ndani ya ligi ikiwa ni timu namba moja yenye mabao mengi kibindoni kwa msimu wa 2024/25. Huyu ni mzawa namba moja kwa utupiaji.

Prince Dube-12

Prince Dube mshambuliaji wa Yanga katupia mabao 12 yeye ni raia wa Zimbabwe. Ukiweka kando kufunga Dube ni mkali kweye kutengeneza pasi za mwisho akiwa na rekodi ya kutengeneza jumla ya pasi 8 za mabao katika kikosi. Jumla Dube kahusika kwenye mabao 20 kati ya 68 yaliyofungwa na Yanga ndani ya ligi.

Leonel Ateba-12

Mshambuliaji wa Simba SC, Leonel Ateba ndani ya ligi katupia mabao 12, alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji, Uwanja wa KMC Complex moja alikuwa ndani ya 18 na moja alikuwa nje ya 18 akimtungua Mohamed Camara kipa wa Pamba Jiji.

Jonathan Sowah-11

Mshambuliaji wa Singida Black Stars ni ingizo jipya ndani ya timu hiyo kwenye dirisha dogo akiwa katupia jumla ya mabao 11. Huyu ni raia wa Ghana timu ya Singida Black Stars ikiwa nafasi ya nne na pointi 53 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 40.

Elvis Rupia-10

Mshambuliaji mwili jumba wa Singida Black Stars Elvis Rupia anaingia kwenye orodha ya wakali wakucheka na nyavu akiwa katupia mabao 10. Huyu ni raia wa Kenya ambaye ana zali lakucheza na nyavu.

Steven Mukwala-9

Mshambuliaji wa Simba SC Steven Mukwala katupia jumla ya mabao 9 huyu ni raia wa Uganda. Katika mchezo dhidi ya Mashujaa FC ugenini nyota huyo alipachika bao la jioni dakika ya 90 akitumia pasi ya Awesu Awesu.

Pacome Zouzoua-9

 Kiungo mshambuliaji wa Pacome Zouzoua anaingia kwenye orodha ya wakali kwenye kutengeneza pasi za mwisho akiwa nazo pasi 9. Sio kwenye kutoa pasi za mabao tu bali hata kufunga ni mkali. Kibindoni ana mabao 9 hivyo kahusika kwenye mabao 18 kati ya 68 yaliyofungwa na Yanga.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.