Kipute cha ligi ya Mabingwa barani Ulaya kuendelea leo ambapo Paris Saint German itawakaribisha Arsenal katika dimba la Parc des Princes nchini Ufaransa kucheza mchezo wa mkondo wa pili baada ya ule wa kwanza uliochezwa April 29 katika dimba la Emirates kumalizika kwa PSG kupata ushindi wa goli moja lililofungwa na Ousemane Dembele Dakika ya nne tu ya mchezo. Goli hilo lililodumu mpaka dakika ya tisini ya mchezo linawapa faida PSG ya kuingia uwanjani leo wakiwa mbele kwa bao moja ambalo walilipata ugenini.
Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Arsenal kukubali kichapo hicho katika uwanja wa nyumbani usiku wa leo watashuka tena dimbani kukabiliana na PSG ambao wao wanafaida ya goli moja mpaka sasa.
Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho Arsenal kufika hatua ya finaili ya ligi ya mabingwa Ulaya ilikua msimu wa mwaka 2005/2006 wakati huo ikiwa chini ya kocha Arsene Wenger ambapo Arsenal ilikubali kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya FC Barcelona.
Kiu ya kucheza Fainali ya Ligi ya mabingwa ulaya kwa mara nyingine tena baada ya miaka kadhaa kupita unaongeza uhondo wa mchezo huu na kuufanya kuwa miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka kote duniani.
PSG nao watakua na kibarua cha kuulinda ushindi huo ili uwape tiketi ya kucheza fainali za ligi ya Mabingwa kwa mara nyingine tena baada ya misimu minne kupita, huku wapenzi wa club hiyo wakiamini wamekua na kikosi bora msimu huu ambacho huwenda kikawaletea kikombe cha Ligi hicho msimu huu.