KUTOKA ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC inakibarua cha kusaka tiketi kutinga fainali Muungano Cup 2025 kwa kusaka ushindi dhidi ya Zimamoto FC saa 1:15 Uwanja wa Gombani, Pemba.
Kwenye robo fainali ya Zimamoto ilikuwa ni Aprili 25 2025 ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Kwenye mchezo huo bao pekee la ushindi lilifungwa na Rashid Salum dakika ya 28. Bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na Coastal Union ikawa imegota mwisho katika Muungano Cup 2025.
Yanga SC ilipata ushindi kwenye mchezo wao wa hatua ya robo fainali dhidi ya KVZ FC baada ya dakika 90 wakawafungashia virago wapinzani wao hao ndani ya uwanja.
Ni Aprili 26 2025 siku ya Muungano Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 ni Aziz Ki alipachika bao la ufunguzi dakika ya 29 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Gombani.
Bao la pili kwenye mchezo huo ni mali ya Dennis Nkane ambaye alianzia benchi alipachika bao hilo dakika ya 85 zikiwa zimesalia dakika 5 mpira kugota mwisho.
Kwenye mchezo huo kiungo Mudathir Yahya alichaguliwa kuwa mchezaji bora ambaye Aprili 29 2025 anatarajiwa kuwa kwenye kazi dhidi ya Zimamoto katika msako wa ushindi.
JKU SC iliyowafungashia virago Azam FC wao wanamsubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Zimamoto vs Yanga saa 1:15. Kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ni tatu zimeondolewa ambazo ni Coastal Union, Singida Black na Azam FC kutoka Ligi Kuu Bara
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.