JKU SC imewaondoa vigogo wawili katika Muungano Cup 2025 ambao wapo ndani ya nne bora Ligi Kuu Tanzania Bara.
Walianza na Singida Black Stars katika hatua ya robo fainali Aprili 24 ilikuwa JKU SC 2-2 Singida Black Stars katika penalti ilikuwa JKU SC 6-5 Singida Black Stars.
Aprili 28 2025, Azam FC waliumaliza mwendo kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Gombani ukisoma JKU SC 2- Azam FC.
Licha ya Azam FC kuanza kufunga mapema dakika ya 15 kupitia kwa Yeison Fuentes bao hilo liligotea dakika ya 50.
Neve Adelin alipachika bao la usawa na bao la ushindi likafungwa na Fredy Seleman dakika ya 80.
JKU SC anamsubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Zimamoto vs Yanga saa 1:15.
Coastal Union, Singida Black na AzM FC kutoka Ligi Kuu Bara zimefunasgiwa virago Muungano Cup 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.