SIMBA SC inayonolewa na Kocha Mkuu Fadlu Davids imetinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa jumla ya bao 1-0 lililofungwa na Jean Ahoua, Uwanja wa Amaan dakika ya 44 kwa pigo la faulo, Aprili 20 2025.
Aprili 27 2025 nchini Afrika Kusini baada ya dakika 90 ubao umesoma Stellenbosch FC 0-0 Simba SC ikiwa ni faida kwa Simba kuandika rekodi kutinga hatua ya fainali.
Kwenye mchezo wa Aprili 27 2025 maamuzi ya VAR yalitumika kwa pande zote mbili kwa Simba SC penalti ilifutwa dakika ya 14 ni Kibu Dennis alionekana kuchezwa faulo ndani ya 18 na kwa Stellenbosch FC penalti moja ilifutwa na bao walilofuga lilifutwa kwa kuwa ilionekana kabla yakufungwa kuna mchezaji wa Stellenbosch FC alikuwa ameotea.
Nahodha Mohamed Hussen wa Simba kwenye mchezo huo Afrika Kusini alionekana akitoa mpira katikati baada ya mwamuzi kuamuru kuwa ni bao kisha akarudisha langoni kwa Camara ili kumpa presha mwamuzi akaangalie VAR.
Baada ya mwamuzi kufanya mawasiliano na VAR uangalizi kukamilika bao hilo lilifungwa na dakika za lala salama ilionekana beki wa Simba amecheza faulo ndani ya 18, mwamuzi akasema hakuna penati ngoma iendelee na mwisho Simba ikatinga hatua ya fainali Kombe la Shirkisho Afrika ikiwa ni mara ya pili kutinga fainali.
Matokeo hayo yataifanya Simba kucheza na RS Berkane ambayo ilimfungashia virago CS Constantine ambapo wataanzia ugenini Morocco na kazi ya pili itakuwa Dar.
Zimbwe amesema kuwa aliwaambia mashabiki kuwa bao moja walilofunga kwenye hatua ya nusu fainali lilikuwa na umuhimu hivyo kutinga kwao fainali ni faida ya bao walilopata nyumbani.
“Niliwaambia watu kuwa bao ambalo tumepata nyumbani ambalo ni moja ni muhimu sana kwenye hatua ya nusu fainali unaona sasa hilo bao limetufikisha hatua ya fainali, tutazidi kupambana kupata matokeo mazuri kwenye fainali.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.