NI Jumamosi ya kazikazi Aprili 26 2025 kuna mechi kali ambazo zinatarajiwa kuchezwa ndani ya Premier League kwa wababe kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.
Miongoni mwa timu hizo ikiwa ni wiki ya 34 ni Chelsea ambayo ipo nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 57 itakuwa kazini kumenyana na Everton iliyo nafasi ya 13 na pointi 38.
Rekodi znaonyesha kuwa wababe hawa walipokutana uwanjani Desemba 22 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Everton 0-0 Chelsea hivyo waligawana pointi na walipokutana Aprili 15 2024 ilikuwa Chelsea 6-0 Everton na Desemba 10 2023 ilikuwa Everton 2-0 Chelsea.
Wababe hawa watakuwa kazini kwa mara nyingine Uwanja wa Stamford Bridge katika msako wa pointi tatu muhimu uwanjani ndani ya dakika 90 zamoto.
Southampton iliyo nafasi ya 20 na pointi 11 baada ya kucheza mechi 33 itawakaribisha Fulham ilyo nafasi ya 9 na pointi 48. Southampton haijawa na mwendo mzuri ndani ya mechi za 2024/25 kutokana na kutopata matokeo chanya.
Baada yakucheza jumla ya mechi 33, ushindi ni kwenye mechi 2 na ilipoteza jumla ya mechi 26 na kupata sare kwenye mechi 5 ndani ya uwanja huku ikiwa inakama nafasi ya mwisho kwenye msimamo.
Wapinzani wao Fulham wapo ndani ya 10 bora kwa kuwa ni nafasi ya 9 kwenye msimamo wapo huku wakipata ushindi kwenye mechi 13, waliambulia kichapo kwenye mechi 11 wakikusanya sare 9.
Brighton yenye pointi 48 nafasi ya 10 itakuwa kazini dhidi ya West Ham yenye pointi 36 nafasi ya 17 kwenye msimamo. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wababe hawa kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.
Kutoka ndani ya tano bora Newcastle United iliyo nafasi ya 5 baada yakukusanya jumla ya pointi 59 itakuwa kibaruani kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Ipswich iliyo nafasi ya 18 na pointi 21 kibindoni.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.