CITY YAKWEA NAFASI YA TATU EPL KWA USHINDI WA KUSISIMUA DHIDI YA ASTON VILLA

Bao la dakika za jioooni kutoka kwa Matheus Nunes limeipatia Manchester City pointi zote tatu nyumbani dhidi ya Aston Villa na kukwea mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Mabingwa hao watetezi wamefikisha pointi 61 kwenye mechi 34 huku Aston Villa wakisalia nafasi ya 7 wakiwa na pointi 57 baada ya mechi 34

FT: Man City 2-1 Aston Villa
⚽ 07’ Silva
⚽ 90+4’ Nunes
⚽ 18’ Rashford (P)