AZIZ KI, PACOME OUT YANGA

KUELEKEA katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Fountain Gate dhidi ya Yanga, kiungo Aziz Ki kuna hatihati akaukosa mchezo huo Aprili 21 2025 kwa kuwa hayupo fiti Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa.

Mbali na Aziz Ki, Pacome naye hajarejea katika ubora huku Musonda Kennedy naye akibainisha kuwa anahisi maumivu kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa wamefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.

“Ni kweli tuna baadhi ya wachezaji majeruhi kama Aucho, Pacome bado hajawa tayari, Musonda anahisi maumivu kidogo si makubwa lakini hatuwezi kumuhatarisha pamoja na Azizi Ki ana maumivu ya muda mrefu.

“Nawaheshimu wachezaji wote. Mimi si kocha wa kulalamika kwamba sina huyu au yule hapana nitampa nafasi kila mchezaji. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo itatuwezesha kufika mwezi Mei tukiwa imara, kwa sababu kila mchezaji atakuwa amepewa muda wa kucheza. Hilo ni jambo muhimu sana kwangu. Asanteni sana.”

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ulisoma Yanga 5-0 Fountain Gate.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.