MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi wapo kamili kuwakabili wapinzani wao Fountain Gate kuelekea mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Aprili 21 2025.
Tayari kikosi hicho kimesepa Bongo kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wao Manyara na mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 5-0 Founatin Gate hivyo Yanga itaingia uwanjani kulinda rekodi huku Fountain Gate wakiwa na hesabu za kutibua rekodi.
Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 67 baada yakucheza mechi 25 i timu namba moja kufunga mabao mengi ambayo ni 64 ikiwa imeshinda mechi 22.
Fountain Gate ni namba mbili kwa timu iliyoruhusu mabao mengi baada yakucheza mechi 26 ikiwa imekusanya jumla ya mabao 47 na pointi zake ni 29.
Miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliopo kwenye kikosi ni Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Ikangalombo, Job Dickson.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.