YANGA WAANDIKA REKODI WAKITINGA NUSU FAINALI

MABINGWA watetezi wa CRDB Federation Cup, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi wameandika rekodi yao kuwa timu iliyopata ushindi mkubwa ndani ya dakika 90 katika msako wa hatua ya kutinga nusu fainali.

Yanga Aprili 15 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Yanga 8-1 Stand United, inatinga hatua ya nusu fainali na itakwenda kukutana na JKT Tanzania.

Ikumbukwe kwamba JKT Tanzania ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Pamba na kwatika mabao hayo hakuna mchezaji aliyefunga hat trick.

Timu nyingine ambayo imetinga hatua ya nusu fainali ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Ni hat trick moja mepatikana kwa timu ambazo zimetinga hatua ya robo fainali kutoka kwa Aziz Ki wa Yanga ambaye alifunga mabao manne mbele ya Stand United.

Ki alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo ambapo beki Ibrahi Bacca alikwama kukamilisha dakika 90 baada ya kupata maumivu kipindi cha pili.

Mabao 9 yalipatikana kwenye mchezo huo ambapo kwa Yanga Aziz Ki alitupia mabao manne dakika ya 16, 51, 60 na 64, Nickson Kibabage dakika ya 20 Clatous Chama ni mabao mawili dakika ya 32 na 41 na bao moja Kennedy Musonda dakika ya 86.

Msenda Senda wa Stand United dakika ya 50 alipachika bao akifuta hati safi kwa kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra akiwa ndani ya 18 kwenye mchezo huo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.