YANGA KUKIPIGA MKWAKWANI, SIMBA MANYARA NUSU FAINALI YA FA

BAADA ya kutinga hatua ya nusu fainali tayari eneo ambalo timu hizo zitachezwa limewekwa wazi hivyo kila mmoja ameshatambua wapi atakuwa kusaka tiketi ya kutinga hatua ya fainali.

Mabingwa watetezi wa CRDB Federation Cup ni Yanga hawa watacheza na JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwenye msako wa mshindi atakayetinga hatua ya fainali.

Ikumbukwe kwamba Yanga imetinga nusu fainali kwa ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Stand United na JKT Tanzania 3-1 Pamba Jiji.

Simba watakuwa Manyara wao walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City watamenyana na Singida Black Stars iliyoshinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.