BAADA ya Singida Black Stars kutinga hatua ya nusu fainali uongozi umebainisha kuwa utapambana kupata matokeo kwenye mchezo wao wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba ili watinge hatua ya fainali.
Mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga, Aprili 15 2025 walikata tiketi yakutiga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Stand United huku Aziz Ki akichaguliwa kuwa mchezaji bora na alifunga mabao manne kwenye mchezo huo.
Singida Black Stars kwenye hatua ya robo fainali mchezo wao ilikuwa ni Aprili 14 2025 ilipata ushindi mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Kaseja Uwanja wa Liti. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Singida Black Stars 2-0 Kagera Sugar watupiaji wa mabao wakiwa ni Victorien Adebayo dakika ya 11 na Jonathan Sowah dakika ya 66.
Watakutana na Simba SC iliyowafungashia virago Mbeya City robo fainali kwa ushindi wa mabao 3-1 Uwanja wa KMC.
Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussen Masanza amebainisha kuwa baada yakushinda mchezo huo wanatambua mshindani wao katika hatua ya nusu fainali atakuwa Simba hilo haliwapo presha wapo tayari kuwakabili.
“Tuna wachezaji imara na kikosi kipo tayari kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Simba kikubwa ni kuona kwamba tunakuwa kwenye mwendelezo mzuri na malengo ni kutinga hatua ya fainali, hii inawezekana na tunavuka hatua hii”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.