MCHEZAJI bora wa mchezo wa Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Prince Dube ameongeza kasi kwenye vita yakuwania tuzo ya kiatu cha mfungaji bora.
Wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex Aprili 10 2025 ukisoma Azam FC 1-2 Yanga, Prince Dube alifunga bao moja dakika ya 33 na bao la ufunguzi lilifungwa na Pacome Zouzoua dakika ya 11.
Bao la Azam FC lilifungwa na Lusajo Mwaikenda dakika ya 81. Dube amefikisha mabao 12 sawa na kiungo mshambuliaji wa Simba Jean Ahoua chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Nyota hawa wawili wote kwa sasa wanakula sahani moja kila mchezaji akiwa na mabao 12 kibindoni. Dube ni mkali wa mabao ya vichwa katika mabao 12 ni sita katupia kwa mapigo ya vichwa huku Ahoua akiwa ni mkali wakutumia mguu wa kulia.
Mabao yote 12 aliyonayo Ahoua ndani ya kikosi cha Simba kafunga kwa mguu wa kulia akiwapa tabu makipa wa ligi ya Bongo.
Ni Clement Mzize jezi namba 10 mgongoni huyu ni mzawa namba moja mwenye mabao mengi akiwa nayo 11 huku Elvis Rupia wa Singida Black Stars akiwa na mabao 10 kibindoni.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 namba moja kwa utupiaji alikuwa ni Aziz Ki alitupia mabao 21 na pasi 8 za mabao.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.