MSAKO wa pointi tatu umezidi kuwa mkali kwa wababe wanaoshuka uwanjani ndani ya uwanja katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, huku Mashujaa wakiwa ni Mashujaa mbele ya Tabora United na Coastal Union wakianza kwa kasi uwanja wa nyumbani, ngoma ilikuwa ni Aprili 10 2025.
Wakiwa Uwanja wa Mkwakwani baada yakufanyiwa maboresho, Coastal Union waliituliza Singida Black Stars kwa kukomba pointi tatu mazima wakiwa nyumbani pale Tanga. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Coastal Union 2-1 Singida Black Stars.
Lucas Kikoti dakika ya 47 alifunga bao lakuongoza likawekwa usawa na Jonathan Sowa kwa mkwaju wa penati dakika ya 76 huku bao la ushindi likifungwa na Bakari Msimu dakika ya 82 zikiwa zimebaki dakika 8 mpira kugota mwisho.
JKT TANZANIA 2-2 NAMUNGO
Uwanja wa Isahmuhyo baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKT Tanzania 2-2 Namungo, mabao yakifungwa na Maka Edward dakika ya 63 na Shiza Kichuya dakika ya 69 kwa JKT Tanzania. Ndani ya dakika 6, JKT Tanzania walifunga mabao mawili wakipindua meza dhidi ya Namungo ambayo ilianza kupata mabao yakuongoza.
Kwa Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda mabao yalianza kufungwa na Saleh Karabaka dakika ya 18 na Fabrince Ngoy dakika ya 49. Nyota Kichuya alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.
MASHUJAA V TABORA UNITED
Uwanja wa Lake Tanganyika nyuki walipoteza makali yao kwa kushuhudia ubao ukisoma Mashujaa 3-0 Tabora United. Mundhir Abdullah alifungua akaunti ya mabao dakika ya 8, Jafari Salum alipachika bao la pili dakika ya 45 na kamba ya tatu ilikuwa ni mali ya David Richard dakika ya 87.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.