UJUMBE HUU KUTOKA JANGWANI WATUMWA KWA MATAJIRI AZAM

CHADRACK Boka, beki wa Yanga ameweka wazi kuwa ushindani ndani ya ligi ni mgumu jambo ambalo linawafanya wawe makini kila wanaposhuka uwanjani kusaka pointi tatu.

Beki huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ndani ya kikosi cha Yanga msimu wa 2024/25, kituo kinachofuata kwa vinara hao wa ligi ni dhidi ya Azam FC, Aprili 10 2025, Uwanja wa Azam Complex.

“Ligi ni ngumu na kuna ushindani mkubwa hilo linatupa nguvu sisi wachezaji kupambana kila mchezo bila kuchoka malengo ikiwa ni kupata pointi tatu muhimu kwenye mechi ambazo tunacheza.”

Boka kacheza jumla ya mechi 20 akikomba dakika 1,394 ni bao moja kafunga ilikuwa kwa pigo huru akitumia mguu wa kulia dhidi ya Pamba mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Februari 28 2025 dakika ya 28.

Katoa pasi mbili za mabao akihusika kwenye mabao matatu kati ya 62 yaliyofungwa na Yanga yenye pointi 64 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.