KUELEKEA kwenye mchezo wa Mzizima Dabi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex kuna mastaa wawili wa kikosi cha Yanga wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika wanakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Azam FC saa 1:00 usiku.
Kuna wachezaji wawili ambao wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo wakusaka pointi tatu ikiwa ni Aziz Ki na Clatous Chama.
Ki alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union kutokana na kutokuwa fiti huku Chama yeye alirejea kwenye mchezo akianzia benchi na alipata muda wakucheza akikomba dakika 7 uwanjani.
Taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa wachezaji hao wapo tayari kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam FC ambao ni Mzizima Dabi mzunguko wa pili kukamilisha dakika 180 kwa wababe hao.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 0-1 Azam FC huku nyota wa Yanga Bacca akiingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka katika kikosi cha Yanga msimu wa 2024/25 kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi alikuwa ni Ahmed Arajiga.
Kiungo Khalid Aucho ataukosa mchezo wa leo kwa kuwa hayupo fiti alipata maumivu ya nyama za paja kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.