MTIBWA Sugar inayotumia Uwanja wa Manungu kwenye mechi za nyumbani wapo siriazi na jambo lao kurejea katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushuka na kuibukia ndani ya Championship.
Timu hiyo kwa sasa ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na jumla ya pointi 60 baada ya kucheza mechi 25 ndani ya ligi msimu wa 2024/25.
Sio kuongoza ligi kwa pointi nyingi timu hiyo ina safu kali ya ushambuliaji ambapo kwenye mechi 25 ilizocheza ni mabao 50 imetupia ikiwa timu namba mbili kufunga mabao mengi vinara ni Mbeya City iliyo nafasi ya pili ikiwa imetupia mabao 51.
Kwenye upande wa ukuta timu hiyo imefungwa mabao 14 ambayo ni machache kwa timu zote ambazo zinashiriki Championship na timu namba mbili ambayo haijafungwa mabao mengi ni Bigman ikiwa imefungwa mabao 15.
Mchezo wao ujao wa ligi ni dhidi ya Mbuni FC unatarajiwa kuchezwa Aprili 12 kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu ndani ya Uwanja.
Mbuni FC ipo nafasi ya 9 ikiwa imekusanya pointi 33 kibindoni baada ya kucheza mechi 25 msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.