BEKI MKALI WA MABAO AZAM FC HUYU HAPA KUKABILIANA NA YANGA

PASCAL Msindo beki wa Azam FC ameweka wazi kuwa kazi kubwa ambayo wanafanya kwenye mechi zote zilizopo mbele yao ni kusaka pointi tatu muhimu kwa kushirikiana na wachezaji wote.

Azam FC itawakaribisha Yanga Aprili 10 2025 kwenye Mzizima Dabi mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni mzunguko wa pili baada ya ule mzunguko wa kwanza ubao kusoma Yanga 0-1 Azam FC.

“Kila mchezo kwetu tunauchukulia kwa umuhimu na malengo ni kupata pointi tatu tukishirikiana wachezaji wote na benchi la ufundi kiujumla.”

Msindo ni chaguo la kwanza ndani ya Azam FC akiwa amecheza jumla ya mechi 23 na kukomba dakika 1,891 uwanjani katika majukumu ya kusaka ushindi.

Mbali na kuwa ni beki nyota huyo ni namba mbili kwa mabeki wenye mabao mengi Bongo akiwa katupia mabao matatu na ametoa pasi moja ya bao.

Hivyo kahusika kwenye mabao manne kati ya 38 yaliyofungwa na Azam FC ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 51 baada ya mechi 25 kakosekana kwenye mechi mbili pekee.

Mkali huyo atakuwa kwenye vita yake kupambania kuongeza rekodi dhidi ya kitasa anayeongoza kwa idadi ya mabao mengi kwa mabeki Ibrahim Bacca wa Yanga ambaye katupia mabao manne msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.