YANGA WASEPA NA TUZO ZAO MAZIMA

WASHINDI wa tuzo ndani ya Ligi Kuu Bara Tanzania ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika kwa Machi wamesepa na tuzo zao mazima baada ya kukabidhiwa Aprili 7 2025 Uwanja wa KMC Complex.

Tuzo hizo walikabidhiwa na wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya NBC benki ya NBC ilikuwa ni kwa Prince Dube ambaye ni mshambuliaji wa Yanga na Miloud Hamdi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa Sheria NBC Edward Lyimo. Ikumbukwe kwamba Aprili 7 2025 Yanga iliwakaribisha Coastal Union kwenye mchezo wa ligi mzunguko wa pili na baada ya dakika 90 ubao ukasoma Yanga 1-0 Coastal Union.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Pacome ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Ni yeye alitwaa tuzo ya mchezaji bora Aprili 2 2025 walipokuwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na baada ya dakika 90 ubao ukasoma Tabora United 0-3 Yanga.

Kwenye msimamo Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 64 baada ya mechi 24 ndani ya msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.