UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa jukumu la kuipeleka Simba hatua ya nusu fainali ni la mashabiki wote hivyo wanapaswa kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa, Aprili 9 2025 kwenye mchezo dhidi ya Al Masry unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni hatua ya robo fainali ya pili baada ya ile ya kwanza kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 nchini Misri.
Simba inapaswa kupata ushindi wa mabao zaidi ya mawili Uwanja wa Mkapa ili kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali huku wakigomea suala la kugotea katika hatua ya robo fainali kwa mara nyingine tena.