BAADA ya mchezo wao uliopita wakiwa ugeneni kupoteza kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Liti ukisoma Singida Black Stars 1-0 Azam FC, kituo kinachofuata ni dhidi ya Yanga.
Matajiri wa Dar kwenye mechi mbili ugenini walipata ushindi mchezo mmoja na kuambulia kichapo mchezo mmoja ambapo ushindi ilikuwa Uwanja wa Sokoine, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Ken Gold 0-2 Azam FC mabao ya Gibril Sillah na Saadun Nassoro.
Sillah amefikisha mabao 8 ndani ya ligi na Saadun ni mabao sita kafikisha ndani ya ligi msimu wa 2024/25 wanakwenda kukutana na Yanga ambayo ina washambuliaji wawili wenye mabao 11, Prince Dube mwenye tuzo ya mchezaji bora Machi na Clement Mzize mwenye tuzo ya mchezaji bora Februari wote wakiwa wametupia mabao 11 kila mmoja.
Katika mchezo wao uliopita ugenini Azam FC ilipoteza dakika ya 74 kwa bao pekee la Elvis Rupia ambaye anafikisha mabao 9 ndani ya ligi akiwa mtupiaji namba moja ndani ya kikosi cha Singida Black Stars.
Yanga mechi zake zote mbili ambazo ni dakika 180 ilipata ushindi ilikuwa Tabora United 0-3 Yanga, Yanga 1-0 Coastal Union, ni mabao manne walifunga na ukuta haujaruhusu kufungwa ndani ya ligi kwenye mechi mbili mfululizo.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex kwenye Mzizima Dabi ilikuwa Yanga 0-1 Azam FC bao pekee la Sillah kwenye mchezo huo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.