AUCHO OUT YANGA,KUWAKOSA AZAM FC

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Khalid Aucho atakosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ni Aprili 10 unatarajiwa kuchezwa ikiwa ni mzunguko wa pili kwenye msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 0-1 Azam FC pointi tatu ilikuwa mali ya Azam FC.

Sababu kubwa ya Aucho kuukosa mchezo huo ni jeraha la nyama za paja ambalo alipata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa KMC Complex.

Taarifa iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu akipambania hali yake.

Get Well Soon.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.