MSAFARA wa Simba uliokuwa nchini Misri mapema Aprili 4 2025 umewasili katika ardhi ya Tanzania baada ya kumaliza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ikiw ni robo fainali ya kwanza.
Aprili 2 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Suez Canal ulisoma Al Masry 2-0 Simba hivyo kibarua kipo kwa wachezaji wa Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids kupambana kupata ushindi wa mabao zaidi ya mawili Uwanja wa Mkapa.
Kikosi cha Simba kimewasili salama ikiwa ni wachezaji wote wakiongozwa na nahodha Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, Leonel Ateba, Ally Salim, Jean Ahoua, Ellie Mpanzu, Kibu Dennis.
Mchezo unaofuata kwa Simba unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 9 2025 ambapo tayari tiketi zimeanza kuuzwa kuelekea mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
Murtanza Mangungu, Mwenyekiti wa Simba amebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanaamini watapambana kupata matokeo mazuri wakiwa nyumbani.
“Tumepoteza kwenye mchezo wa ugenini bado tuna mchezo mwingine nyumbani tuna amini kwamba huu tutapata matokeo mazuri na kusonga hatua ya nusu fainali, mashabiki wajitokeze kwa wingi.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.