PACOME Zouzoua kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kila mechi ni ngumu wakiwa uwanjani wanapambana kufanya vizuri kupata matokeo ndani ya uwanja nyota huyo balaa lake sio dogo kutokana na kuwa katika ubora kwenye mechi anazocheza uwanjani.
Aprili 2 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma Tabora United 0-3 Yanga, mabao ya Israel Mwenda, Clement Mzize na Prince Dube yalitosha kuipa pointi tatu Yanga.
Pacome alitoa pasi kwa Mzize dakika ya 56 kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 ikaleta bao la pili baada ya shambulizi la kushtukiza na alitoa pasi ya pili kwa Dube dakika ya 67 akiwa nje ya 18 kwa mguu wake wa kulia hali iliyopelekea kuhusika kwenye mabao mawili kati ya matatu.
Yanga inakuwa ni timu namba moja kufunga mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 61 na safu washambuliaji wake wawili Mzize na Dube kila mmoja katupia mabao 11 kwenye ligi.
Pacome anafikisha jumla ya pasi 8 za mabao ndani ya ligi akiwa ni namba mbili kwa mastaa wenye pasi nyingi huku kinara akiwa ni Feisal Salum wa Azam FC mwenye pasi 12 kibindoni.
Kiungo huyo amesema: “Kazi bado inaendelea furaha kubwa kuona kwamba tunapata ushindi kwani mchezo wetu dhidi ya Tabora United hakuwa mwepesi tulikutana na timu ngumu yenye wachezaji wazuri.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.