LIGI Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika inaendelea mzunguko wa pili ambapo kuna wababe watakuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90 za kazi.
Ni JKT Tanzania iliyo nafasi ya 6 kwenye msimamo baada ya mechi 23 huku safu ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 18 na ukuta kuruhusu mabao 17 na pointi zao kibindoni 30 itawakaribisha Dodoma Jiji, Uwanja wa Isahmuhyo, Dar saa 10:00 jioni.
Dodoma Jiji kwenye msimamo nafasi ya 8 pointi 27 baada ya mechi 23, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 22 na ukuta umeruhusu jumla ya mabao 33 kufungwa ndani ya uwanja.
Ken Gold iliyo nafasi ya 16 na pointi 16 baada ya mechi 23 itawakaribisha matajiri wa Dar Azam FC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya saa 10:00 jioni.
Kagera Sugar iliyo nafasi ya 14 na pointi 19 itamenyana na Coastal Union iliyo nafasi ya 10 na pointi 25 itakuwa ni Uwanja wa Kaitaba, Kagera inatarajiwa kuchezwa saa 1:00 jioni.
SIMBA KUWAKABILI MASHUJAA
Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids ndani ya Aprili hawatakuwa na mchezo wa ligi kete yao itakuwa dhidi ya Mashujaa hii inatarajiwa kuchezwa Mei 2 2025, Uwanja wa KMC Complex, Dar.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.