FADLU Davids, Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba ambacho kinapeperusha bendera ya Tanzania kimataifa amesema hesabu kubwa ni kuona wanapata matokeo chanya kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri ambao unatarajiwa kuchezwa leo saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo nchini Misri ni Moussa Camara, Ally Salim na Hussen Abel kwa upande wa makipa na washambuliaji ni wawili Leonel Ateba na Steven Mukwala huku Kibu Dennis, Yusuph Kagoma wakiwa baadhi kwenye eneo la viungo na nahodha Mohamed Hussen Zimbwe Jr yupo kwenye eneo la mabeki.
Robo fainali ya kwanza Simba watakuwa ugenini na ile ya pili watakuwa Uwanja wa Mkapa Aprili 9 ambapo mshindi wa jumla kwenye mchezo huo atakata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Fadlu ameweka wazi kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo jambo ambalo lipo wazi kwenye hatua hiyo ambayo ni ngumu kwa kila timu kutokana na ubora.
“Tumefanya maandalizi kwa muda wa siku nne tuna amini kwaba utakuwa ni mchezo mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya kuona kwamba tunapata matokeo tukiwa ugenini katika mchezo wetu muhimu na wachezaji wapo tayari.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.