ROBO fainali ya kwanza Al Masry 2-0 Simba ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali, Uwanja wa Suez Canal.
Abderrahim Deghmoum alianza kupachika bao la uongozi dakika ya 15 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 likimshinda Moussa Camara na kamba ya pili ni mali ya John Okeyo dakika ya 89.
Ellie Mpanzu alikuwa na majukumu ya kupiga kona ambapo alifanya hivyo dakika ya 14, 39, 43, 57 na 86 hazikuwa na faida kwa Simba na alichezewa faulo dakika ya 37 na Ahmed Aid ambaye alionyeshwa kadi ya njano.
Kete ya maamuzi ya mwisho ni Uwanja wa Mkapa, Aprili 9 2025 ambapo Simba wanadeni kupata mabao zaidi ya mawili ili kusonga hatua ya nusu fainali.
Katika safu ya ulinzi Simba dakika 15 za mwanzo na dakika 15 za kipindi cha pili mwishoni walikosa utulivu hali iliyowapa wapinzani wao Al Masry kutumia makosa ambayo walifanya kupata mabao hayo.
Eneo la ushambuliaji hakukuwa na utulivu kwa Leonel Ateba ambaye alianza kikosi cha kwanza huku Steven Mukwala ambaye aliingia kipindi cha pili naye akikwama kufungua ukurasa wa mabao licha ya Simba kucheza kwa utulivu kipindi cha pili.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.