KOCHA Mkuu wa Liverpool, Arne Slot ameweka wazi kuwa mchezo wao wa Merseyside Derby lazima wapambane kupata ushindi huku kikwazo kikitajwa kuwa ni David Moyes ambaye ni Kocha Mkuu wa Everton kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Anfield.
Huu ni mchezo wa Ligi Kuu England ambapo vinara hao wa ligi wakiwa na pointi 70 baada ya kucheza mechi 29 watakutana na wapinzani wao Everton walio nafasi ya 15 na pointi 34 kibindoni kwa msimu wa 2024/25.
Ikumbukwe kwamba Liverpool kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao na Newcastle ilikwama kupata ushindi ikiwa chini ya Slot jambo lnaloongeza ugumu kuelekea mchezo wa leo.
“Niliwaambia wachezaji kwamba hatukuwa kwenye ubora mchezo wetu uliopita na sasa tunapaswa kufanya kazi kubwa kwenye mchezo wetu wa Derby kwa kuwa huu sio mchezo wa kawaida.”
Everton inayonolewa na Kocha Mkuu, David Moyes inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na pointi 17 mbele ya eneo la kushuka na kwa timu iliyozoea kupoteza wakati wa Sean Dyche alipofutwa kazi, sasa hawajashindwa kwenye ligi tangu usiku wa baridi kali mapema Januari.
Ni mabadiliko ya kushangaza ambapo Moyes ameshangaza kila mtu katika klabu na kwingineko pamoja na yeye mwenyewe jinsi bahati yao imebadilika haraka. Wametoka kwa timu ya kulala hadi kushuka daraja hadi moja ambayo sasa inapaswa kuwa na matumaini ya kweli ya nusu ya juu mwaka ujao.
MECHI NYINGINE HIZI HAPA
Newcastle United v Brentford
Manchester City v Leicester City
Bournemouth v Ipswich
Brighton v Aston Villa
Southampton v Crystal Palace