SIMBA KAMILI KUWAKABILI WAARABU/ ORODHA HII HAPA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wao dhidi ya Al Masry na wameanza na mazoezi muda mfupi baada ya kufika Misri ili kuwa imara kwenye dakika 90 za ushindani.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa jambo ambalo linawafanya wafanye maandalizi kwa umakini zaidi.

“Tumefika salama Misri na kila kitu kinakwenda salama tunamshukuru Mungu ambapo tayari tumeanza maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Al Masry.

“Tulicheza mchezo wetu Machi 27 dhidi ya Big Man hivyo tunaendelea na mazoezi kuwa imara kwa muda wa siku nne na wachezaji wote ambao tumekuja nao wapo tayari na tumeanza mazoezi mapema baada ya kufika.

“Habairi nyingine njema ni kwamba tumeruhusiwa kutumia Uwanja wa Mkapa mchezo wetu dhidi ya Al Masry ambapo awali ulifungiwa mpaka pale utakapofanyiwa marekebisho tunaishukuru Serikali kwa kufanya juhudi za dhati.

“Baada ya kufanyiwa ukaguzi kwa mara nyingine tena umekidhi vigezo hivyo tunakwenda kufanya kazi kwa nguvu kwenye mchezo wetu ujao, nipende kuwaambia mashabiki wa Simba kuwa mnyama anarejea Uwanja wa Mkapa.”

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 9 2025 ambapo mshindi wa jumla kwenye mchezo huo atakata tiketi kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

HII HAPA ORODHA YA WACHEZAJI WALIOPO MISRI

Moussa Camara, Ally Salim na Hussen Abel kwa upande wa makipa.

Mabeki ni Karaboue Chamou, Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, Valentine Nouma, David Kameta, Kelvin Kijili.

Viungo ni Yusuph Kagoma, Fabrince Ngoma, Elie Mpanzu, Deborah Fernandez, Ladack Chasambi, Kibu Dennis, Awesu Awesu, Jean Ahoua, Augustine Okejepha na Joshua Mutale.

Washambuliaji ni Leonel Ateba na Steven Mukwala.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.