SIMBA, YANGA ZAGONGANA KWA MSHAMBULIAJI MGHANA

WATANI wa jadi Simba na Yanga kwenye hesabu za kuboresha eneo la ushambuliaji inatajwa kuwa wamegongana kuwania saini ya raia wa Ghana, Jonathan Sowa ambaye yupo ndani ya kikosi cha Singida Black Stars.
Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya Singida Black Stars amekuwa imara kwenye eneo lakutupia mabao ambapo kwenye mechi ambazo amecheza zikiwa hazijafika 14 katupia mabao 7 ndani ya ligi.
Miongoni mwa timu ambazo alizifunga ni pamoja na Yanga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex ubao uliposoma Yanga 2-1 Singida Black Stars alimtungua kipa namba moja Djigui Diarra.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Yanga wapo kwenye hesabu za kuinasa saini ya mshambuliaji huyo na Simba nao wanatajwa kuwa kwenye rada za kumfuatilia nyota huyo.
Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Singida Black Stars alisema kuwa kwa timu ambazo zinahitaji huduma ya mchezaji Sowa kwa sasa zinapaswa zitulie kwani wanampango naye bado.