KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids alfajiri ya Machi 28 2025 kimekwea pipa kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi yaAl Masry, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025.
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Machi 9 Uwanja wa Mkapa ambapo Simba watakuwa nyumbani na wamebainisha kuwa kikubwa ambacho kinhitajika.
Kwenye msafara wa wachezaji waliosepa Bongo katika eneo la mlinda mlango ni Mousa Camara, Hussen Abel hawa walikuwa kwenye msafara uliaza safari leo huku Aishi Manula akiwa hayupo kwenye mpango kazi.
Ally Salim yeye atajiunga na timu kambini akitokea timu ya taifa ya Morocco baada ya kuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa Morocco na Stars kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao licha ya kila timu kupambana kusaka ushindi.
“Tuna kazi kubwa kwenye anga la kimataifa kwa kuwa hii ni hatua kuna ushindani mkubwa, Aishi Manula alipata maumivu il kwa sasa anaendelea vizuri ndio maana ulimuona kwenye mchezo wetu dhidi ya Big Man akianzia benchi lengo ni kumrejeshea utimamu wa mwili.”
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni Joshua Mutale, Nouma,Duchu, Mousa Camara, Joshua Mutale, Ellie Mpanzu.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.