Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa kutumika kwa michezo inayosimamiwa na Shirikisho hilo baada ya Ukaguzi uliofanywa na Wakaguzi wa CAF mnamo Machi 20, 2025.
Taarifa ya leo Machi 28, 2025 iliyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imeeleza kuwa CAF inaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea kwenye uwanja huo.
Uwanja sasa upo tayari kutumika kwenye michezo ya robo fainali na nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) 2024/2025 huku Simba Sc ikitarajiwa kuutumia kwenye mchezo wake wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry.